Kwa
ukakamavu kijana wa CCM akimvisha kitambaa Mh.Mwigulu nchemba mara baada
ya kuwasili kwenye kambi ya mafunzo ya vijana wa CCM-Namtumbo
CCM oyeeeeee!!!Naibu katibu mkuu akisalimiana na vijana wa CCM wakati akiingia eneo la tukio.
Naibu katibu
mkuu wa CCM Tanzania bara ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi
Mh.Mwigulu Lameck Nchemba leo Tar.31/10/2013 amefunga rasmi mafunzo ya
vijana wa CCM (UVCCM) yaliyofanyika kwa muda wa wiki mbili hapa Ruvuma
Wilaya ya Namtumbo.Mafunzo haya yaliyojumuisha wilaya zote za Ruvuma kwa
vijana wa CCM yalilenga kuwajengea uwezo vijana wa kutambua Umuhimu wao
katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ndani ya nchi yao,siasa
za nchi na mwenendo wake,Uelewa kuhusu namna ya kufanya maamuzi sahihi
katika umri wake huu wa ujana,pia kuwaandaa kifikra na kimaadili
kwaajili ya kuijenga na kuimarisha CCM pamoja na jumuia zake hasa Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
Vijana wakiwa na nyuso za Furaha baada ya kuonana uso kwa uso na Kiongozi wao wa chama wa ngazi ya taifa.Mh.Mwigulu nchemba
Akizungumza
kwa mifano mingi iliyohai ndani na nje ya nchi yetu,Mh.Mwigulu Nchemba
wakati wa kufunga mafunzo ya vijana wa CCM amezungumza na vijana wote
waliokuwepo kambini(Vijana 450) na kuwasihi sana kuwa makini na mambo
makuu matatu,Moja ni kuhusiana na Uandishi wa katiba mpya,Pili
amezungumzia kuhusu rasilimali za nchi na mwisho amesisitiza kuhusu
Umuhimu wa vijana kujitambua hasa ukizingatia Taifa letu linapita katika
kipindi aambacho vijana ni wengi sana kuliko rika lolote lile.
Hapo vipiiii???ni ishara ya dole(mambo sawa) kutoka kwa Naibu katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi.
Akianza kwa
kuzungumzia Mchakato wa uandishi wa katiba Mpya,Mwigulu Nchemba
amewaomba vijana kuwa makini sana na propaganda zozote zile
wanazozisikia kutoka kwa watu wengine kuhusu kufanya vurugu ili katiba
isipatikane.Amesema mchakato wa katiba umekwenda vizuri na umezingatika
matakwa ya kila kundi na Taasisi licha ya Taasisi zingine kutaka maoni
yao yawe bora kuliko ya watu wengine,"Katiba hii si ya CCM na sio ya
chama chochote kile au mtu yeyote yule ni katiba ya Watanzania wote bila
kuangalia rangi,kabila,chama,maumbile ya mtu n.k .Maoni yamekusanywa na
kufanyiwa tathimini na tume husika na sasa tunaelekea hatua za mwisho
za kupata katiba mpya.Hivyo basi nawaomba sana vijana wa CCM na vijana
wengine wote kuacha kujiingiza kwenye makundi na mkumbo wa kugomea
mchakato wa katiba mpya,kwa sababu hao wanaowahimiza kugoma wao wenyewe
wanaajenda yao ya siri kuhusu Taifa hili.Ni kawaida yao kugoma,ni
kawaida yao kupinga kila kitu,Kila mmpja wetu alipewa nafasi ya kutoa
maoni kupitia taasisi na wanachama wake,Kuna wenzetu walikuwa wanafanya
mikutano ya hadhara,hii yote ni kuhadaa na kudanganya
watanzania."alisema.
Namshukuru
sana Rais kikwete kwa kuwapa somo wapinzani kwamba maandamano si
suruhisho na jambo lolote zaidi ya kudumaza maendeleo,Yawezekana
walikuwa natafuta sehemu ya kula ruzuku za vyama vyao sijui!!Lakini
tujiulize ni mapenzi gani haya ya jioni?Ni ndoa gani hii ya watu watatu
ya usiku?Wapi na wapi hawa watu wakaungana eti kutetea maslahi ya
Watanzania.?.
Hivyo
nawaomba sana vijana muache kabisa kabisa kujihususisha na uvunjifu wa
amani au kugomea jambo lolote la kitaifa.Kama linakwenda vibaya vyombo
vya kusemea vipo na serikali inawapa nafasi hiyo.
Jambo kuwa
nawahakikishieni vijana wa CCM,Kwa namna CCM tulivyoimara iwe kwa katiba
ya sasa au mpya au katiba yoyote CCM tutashinda kwa sababu
tunajiamini,tunakubalika kwa watanzania,tunamtandao mkubwa sana na
jumuia yetu moja tu kama hii ya vijana ni kubwa kuliko CHADEMA yote na
vyama vingine.
Vijana wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi Mh.Mwigulu Nchemba
Jambo la
pili Mh.mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu rasilimali za nchi na namna
vijana wanatakiwa watumie fursa husika kuzilinda mali na kujitengenezea
mazingira ya ajira kwa siku za karibuni.Mwigulu amewasisitizia vijana
kuwa serikali imejenga barabara kutoka Dsm hadi Namtumbo kwa kiwango cha
rami na barabara hiyo imeunganishwa mikoa yote ya Tanzania.Hivyo
rasilimali za nchi ni lazima zilindwe ilikunufaisha wazawa/watanzania
wote na sio watu wachache.Ameomba vijana kulinda rasilimali za nchi yao
na kauchana na wajasiliamali wa mataifa makubwa ambao wamekosa uzalendo
ndani ya nchi yetu na wanaingia mikataba ya vyama vya nje ya kuwapa
masharti eti wakichukua dola watagawana rasilimali zilizopo.
Naibu katibu mkuu akitoa kadi ya uanachama wa UVCCM kwa mmoja wa vijana wa CCM waliohudhuria mafunzo hapa Namtumbo.
Swala la
ulinzi na usalam wa Taifa letu ni la kila mmoja wetu vijana,hakuna
kuwapa nafasis watu wasio litakia mema taifa letu.Serikali ya CCM
imejipanga kuhakikisha rasilimali zilizopo zinanufaisha wananchi
wote.zinalindwa kwa namna yoyote ile.Nimesikia kuwa kuna wasiasa
wanakuja kuwaomba mfanye maandamano na vurugu kuhusu mali za nchi
yenu,Wapuuzieni hao kwasababu nyie wenyewe mnaona kazi zinazofanyika na
serikali yenu na namna rasilimali zinavyotumika kwa manufaa yoyote.Hapa
Namtumbo na mkoa mzima wa Ruvuma miradi ya serikali ya mingi
imeshatekelezwa ya barabara,Umeme na afya ambayo ni kazi ya serikali ya
CCM kupitia kodi na manufaa ya rasilimali zetu.Naomba sana mtumie ujana
wenu kulinda mali za nchi na kuipigania CCM iendelee kuongoza nchi yetu
kwa miaka mingi zaidi kwa sababu nje ya CCM vyama vingine ni wababishaji
tu na wanajenda zao na ndugu zao huko kwenye mataifa ya nje.
Mh.Mwigulu Nchemba akizungumziza na mamia ya vijana wa CCM wakati wa kufunga mafunzo.
Msiwe kama
watu wa Misri ambao hadi leo hawalewi wanachokihitaji,kwa sababu
walimuondoa Rais wao wa aliyekuwepo madarakani,wakamuweka wakwao,ndani
ya miezi sita wamemng'oa waliomuweka wanasema bora yule wa kwanza.Leo
hii ukiwauliza wanataka nini watakwambia hata hawajui wanataka nini.Nchi
yao imeshagawanyika na amani hairudi tena kirahisi.
Tatu,Naibu
katibu Mkuu ametoa somo kwa vijana wa CCM namna ya kuendana na hali
halisi ya Taifa letu hasa idadi kubwa ya vijana kuliko rika lolote ndani
ya nchi.Vijana ni wengi sana na wengi hawana ajira za kutosheleza
mahitaji yao.Hivyo wingi wa vijana,Mh.Mwigulu anasema ni lazima vijana
watumia muda na akili zao vizuri ilikuepukana na makundi hatarishi ya
tabia na maisha yao,kujiepusha na vyama vinavyohangaika huku na kule
kuhakikisha nchi yetu haitawaliki.
Zaidi
ya vijana wa CCM 450 waliokaa kambi wiki mbili kujifunza namna ya
kuongoza,siasa na utendaji wakimsikiliza Mh.Mwigulu Nchemba.
Nanukuu"Nimekuwa
kijana kama nyie,nimepitia umoja wa vijana wa chama changu cha
CCM,Nilijituma kujihusisha na kazi za maendeleo ya chama na nchi
yangu,Niliepukana na makundi yasio na tija kwangu na nilitii kile
wakubwa walichonielekeza ndio maana leo nimefikia katika hatua kubwa
kama hii ya uongozi nikiwa bado kijana"Hivyo basi nanyie mnayonafasi ya
kuhakikisha mnakuwa watu wema katika jamii yetu,mfano wa kuigwa,na hasa
nategemea mafunzo haya yamewapa somo kubwa sana na mmeelimika vya
kutosha namna ya kuwakiongozi na mtendaji mzuri kuanzia ngazi ya
familia,Shina,tawi n.k kwa CCM.
Mh.Mwigulu
Nchemba akimtunuku mmoja wa vijana wa CCM, kuthibitisha kuwa
amehudhuria mafunzo ya utendaji na uongozi wa umoja wa vijana.
Umoja wa
vijana ndio siraha ya chama,mnategemwa sana kuzalisha viongozi wajao
kutoka kwenye kundi hili.Nimeshawaona warithi wa Komba
hapa(uimbaji),warithi wa Jenista Mhagama(uongozi) akina Dr,Emmanuel
Nchimbi wapo hapa na hata Mh.Vita kawawa wingine yupo hapa.
Hivyo basi
mnakila sababu ya kuendelea kuitetea CCM na kuhakikisha mnalinda heshima
yake kwa nchi na nje ya nchi.hatupendi CCM kuwa kama vyama vingine
ambavyo wezi wastaafu,wazinzi,mwenyekiti wake anapigana ngumi na
mwenyekiti mwenzake hao wote kwao wanajiita makamanda na majembe.
Mh.Mwigulu nchemba akisalimiana na kuzungumza machache na moja ya Mzee wa CCM anayeishi wilaya ya Namtumbo-Ruvuma.
CCM tunahitaji kuona makamanda wakweli na majembe ya kweli kama akina Nape Moses Nnauye,Sixtus mapunda na vijana wote wa UVCCM na viongozi wake wakizaliwa kutoka miongoni mwenu vijana wa Ruvuma.
Ni rai yangu
kwako kijana wa CCM na wakitanzania kuwa baada ya mafunzo haya kila
mmoja wenu atakwenda kuwa mwalimu kwa mwenzake huko muendako.CCM ipo
pamoja nanyi na hatuwezi kuipoteza benki hii ya vijana na tunaanza
miradi mbalimbali ya chama kupitia kwenu.
Mbunge wa Namtumbo Vita kawawa akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu nchemba
Naye,Mbunge
wa Namtumbo Mh.Vita Kawawa aliyekuwa mwenyeji wa Mh.Naibu katibu mkuu
alizungumza na vijana waliomaliza mafunzo yao kwa kuwambia "Wote mliopo
hapa mmeona maendeleo yanayofanyika huku Ruvuma na hasa hapa
Namtumbo,Mwaka 2010 hatukuwa na rami wala umeme,Leo tuna rami na umeme
hapa.Naomba uchaguzi ujao muwe vinara wa kuifanya CCM iendelee kuongoza
jimbo hili na dola ya nchi yetu.Vijana wenzangu huu ni muda wa kupambana
sana na wapinzani wetu,hawana sera zaidi ya kusuka mipango ya kuharibu
amani ya nchi na kufanya nchi isitawalike.Ilani ya CCM imetekelezwa
ipasavyo na mnahaki ya kusimama na kuitetea CCM popote pale.Nipo tayari
kuwasaidia kufanya mipango endelevu ya kujenga chama pamoja nanyi vijana
wenzangu".
Mbali na
kuwa mgeni rasmi kwenye kufunga mafunzo ya vijana wa CCM hapa
Namtumbo,Naibu katibu mkuu alipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa ofisi
za chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo,ofisi kubwa wenye kujuisha
jumuia zote za chama,car wash,Ukumbi wa mikutano na maeneo ya
biashara(miradi ya chama).
Mh.Mwigulu
Nchemba akiingia kwenye ofisi za CCM wilaya ya Namtumbo,ofisi mpya
ambazo bado zinaendelea kujengwa.Kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya
Namtumbo.
Mwigulu
alitumia fursa hiyo kuwapongeza sana viongozi wa chama kuanzia ngazi ya
mkoa,wilaya na had ngazi ya chini kabisa kwa namna wanavyoendelea
kuijenga CCM na kuiimarisha ndani ya mkoa wa Ruvuma.
Wilaya ya
Namtumbo ni mpya ikiwa na miaka saba(7) sasa tangu ianzishwe na Mbunge
wake ni Vita Kawawa ambaye alikuwa mwenyeji wa Mh.Mwigulu Nchemba siku
ya leo.CCM inashikilia kata zote za wilaya ya Namtumbo na inashikiliza
vijiji vyote (serikali za mitaa).Hivyo CCM ndicho chama pekee
kinachoongoza wilaya nzima ya Namtumbo.
Naibu
katibu mkuu akipewa maelekezo kutoka kwa katibu wilaya ya Namtubo wa
CCM kuhusu maendeleo ya ujenzi wa ofisi za kisasa za chama.
Mapenzi kwa chama kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.Mh.Mwigulu alimzawadia hicho alichokishika mtoto mkononi.
Pia alipata
wasaha wa kukutana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh.Said Thabit Mwambungu
ambapo walizungumzia hali ya maendeleo ya wilaya na hali ya kisiasa
ndani ya mkoa wa Ruvuma.
Naibu
katibu Mkuu alipomtembelea Dc wa wilaya ya Namtumbo ofisini kwake kabla
ya kuelekea kwenye ufungaji wa mafunzo ya vijana wa CCM.
0 comments:
Post a Comment