Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitolea ufafanuzi wa kina kwa
Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma mapema leo
jioni,kuhusiana na tatizo sugu la bei ya zao la Korosho kwa
wakulima,ambao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu,Kinana
aliwahakikishia Wanachi hao kuwa tatizo hilo watalifanyia kazi ipasavyo
na kufikia hatua ya kulimaliza kabisa.
Aidha
tatizo hilo ni kubwa kwa upande wa mikoa ya Kusini,ikiwemo Mtwara,Lindi
na Ruvuma.Kinana alibainisha kuwa CCM kitahakikisha suala la hilo
linashughulikiwa kwa umakini mkubwa ikishirikiana na Serikali sambamba
na sambamba na taasisi zinazohusika na zao hilo,ili kukomboa uchumi wa
Wananchi wa eneo hilo hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kubangua korosho
vinajengwa na vile ambavyo vimebinafsishwa na havifanyi kazi
kunaandaliwa utaratibu ambao utawafanya wawekezaji wengine kupewa ili
vifanye kazi na kutatua tatizo la bei ndogo ya zao hilo inayolipwa na
wanunuzi.
Katika
ziara hiyo hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC siasa,Itikadi na
uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Dkt.AshaRose Migiro.
Baadhi
ya Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
wakishangilia jambo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman
Kinana,kuzungumzia na kufafanua vyema kuhusiana na tatizo kubwa lililopo
kwenye zao la Korosho,ambako kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi ikiwemo suala la bei ya ununuzi wa Korosho kuwa ndogo,malipo
kutokulipwa kwa wakati kwa wakulima na mengineyo.
Mbunge
wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ,Mh.Ramo Matalla Makani akielezea baadhi
ya matatizo yanayoisumbua Wilaya hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana (pichani kulia) mapema leo,katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye kijiji cha Nakapanya,Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.Kinana na
ujumbe wake wataanza ziara yao rasmi leoo Wilayani humo mkoani Ruvuma
kwa madhumuni ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa Ilani ya CCM,katika Mikoa ya Ruvuma na Mbeya.
Baadhi
ya Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa
wamekusanyika mapema jana wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana,alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na ufumbuzi wa
matatizo yao mbalimbali ikiwemo suala la huduma za afya,Barabara,Maji
sambamba na tatizo sugu la zao la Korosho wilayani humo.
Michuzi blog
Michuzi blog
0 comments:
Post a Comment