ASIYEKWENDA NA KASI YA SERIKALI KUTOVUMILIWA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema, serikali haitamvumilia na kumuonea huruma mkurugenzi wa halmashauri, mji, manispaa na jiji ambaye atashindwa kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Mbali na hilo, Naibu Waziri amewaagiza wakurugenzi wote hapa nchini kutumia rasilimali za msitu zilizoko katika wilaya zao kumaliza tatizo la madawati na kusema kwamba hakuna mwanafunzi yeyote atakayekaa chini kwa kukosa dawati.
“Agizo hili ni la serikali ya awamu ya tano, sisi hatuangalii wapi ni lazima uwajibike pale unapoona mambo hayaendi vizuri, hata mkurugenzi wangu na wewe agizo hili linakuhusu, mkurugenzi tumia rasilimali za miti zilizoko katika halmshauri yako kupunguza tatizo la madawati kama lipo,” alisema Ngonyani.
Naibu Waziri ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na madiwani na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Namtumbo katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Alisema amepiga marufuku tabia ya madiwani kufanya biashara na halmashauri kwa kuwa jambo hilo linaweza kuleta mtafaruku kwa halmashauri na hivyo kushindwa kukamilika kwa miradi ya maendeleo.
Alisema hata yeye japokuwa ni mbunge wa jimbo hilo, hatoweza kufanya biashara Na halmashauri kwani ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma hivyo kila kiongozi kuanza kujitafakari nafasi aliyonayo kwa wananchi.
Aidha amewataka madiwani hao kuhakikisha kwamba wanashirikiana na watumishi wa halmashauri kupunguza tatizo la uhaba wa matundu ya choo, madawati na upungufu wa zahanati katika maeneo yao.
CHANZO ; HABARI LEO.

WANAWAKE WAHAMASISHWA KULETA MAENDELEO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WANAWAKE wilayani Songea, Ruvuma wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi hapa nchini kwa kuwa mfano bora katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo.
Wameelezwa wakifanya hivyo, itawawezesha kubadili mawazo na mtazamo kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu anayehitaji kusaidiwa kwa kila kitu katika maisha yake.
Mbali na hayo, wameaswa kutumia uwezo wao kuibadili jamii ya kitanzania kitabia na kifikra dhidi ya mtazamo kwamba mtoto wa kike ndiye anayeongoza katika suala zima la mmomonyoko wa maadili, unaosababishwa na kuingia kwa utandawazi.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na diwani wa Ndilimalitembo katika Manispaa ya Songea, Cresensia Kapinga, wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali wa kata hiyo wanaojishughulisha na biashara ndogo ikiwemo matunda na mboga.
Alisema hivi sasa kuna vitendo vya mmomonyoko mkubwa wa maadili hapa nchini ambapo vijana wanaiga mienendo ya kigeni na wakati na kuacha mila na desturi ya Mtanzania, jambo ambalo ni hatari.
Kwa mujibu wa Kapinga ni kwamba vitendo hivyo vinahitaji nguvu ya pamoja kwa wazazi na walezi na hata kwa jamii husika kwa sababu tayari imeonekana katika baadhi ya familia mzazi anashindwa kukemea tabia hizo na kusababisha vijana wengi kuangamia.
Alisema asilimia kubwa ya watoto wa kike wanaambukizwa virusi vya Ukimwi na vijana wa kiume wanaingia katika matumizi zaidi ya dawa za kulevya.
CHANZO ; HABARI LEO.

Mbunge Kessy ataka serikali ibane matumizi zaidi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Mbunge wa Nkasi kaskazini Ally Keissy amewataka wabunge waungane kukataa matumizi ya serikali kuwaleta wakurugenzi,wakuu wa mikoa pamoja madereva kwenda Dodoma kushiriki vikao vya Bunge kwani fedha nyingi hupotea bila mafanikio kuonekana.

Kessy ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11.

''Huu utaratibu wa kuwaleta madereva, na wakurugenzi pamoja na wakuu wa mikoa ni lazima wabunge tuungane kupinga matumizi yasiyo ya lazima,hapa na tuanze na hawa maana kuwasafirisha wakuu wote hawa nchi nzima kuja Dodoma hizo fedha zingeelekezwa katika sehemu nyingine kusaidia miradi ya wananchi''Amesisitiza Kessy.

Aidha Kessy ameiomba serikali kumuunga mkono jimboni kwake katika kwenda kuhakiki fedha zilizotumwa kwa ajili ya miradi ya maji na mbolea kwa wakulima kwani fedha nyingi zimeliwa.

MWALIMU AKUTWA AMEJINYONGA CHUMBANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Peramiho, Songea mkoani Ruvuma, Baraka Mwakajila (29), amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shati ndani ya nyumba alimokuwa akiishi.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea juzi saa sita mchana katika mji mdogo wa Peramiho, nje kidogo ya Manispaa ya Songea.
 
Malimi alisema inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Rashid Pilly, aligundua kujinyonga kwa mwalimu huyo, baada ya kupita eneo la nyumba aliyokuwa anaishi na kuona nzi wengi wametapakaa kwenye eneo la dirisha la chumba alichokuwa analala.
 
Alifafanua zaidi kuwa Mwalimu Pilly baada ya kuona hali hiyo, alisogea hadi mlangoni na kukutwa mlango ukiwa umefungwa huku eneo hilo likiwa na harufu kali iliyoashiria kuna kitu ambacho kimeoza.
 
Alisema baadaye Mwalimu Pilly alilazimika kwenda kutoa taarifa kwenye kituo kidogo cha Polisi cha Peramiho na baadaye askari polisi wakiwa wameongozana na mganga, walifika eneo la tukio.
 
Baada ya kufika, alisema walivunja mlango na kuingia ndani ya nyumba hiyo ambako walimkuta Mwalimu Mwakajila akiwa tayari ameshakufa muda mrefu baada ya kujinyonga.
 
Alisema Mwakajila alijinyonga ndani ya nyumba ambayo ni mali ya shule na askari walikuta barua chini ya sehemu aliyojinyongea iliyokuwa imeandikwa Januari 4 mwaka huu na mwanamke (jina linahifadhiwa), anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, ambaye alimtaka aachane naye na aendelee na maisha yake.
 
Malimi alisema polisi baada ya kuiona na kuisoma, waliendelea kuufanyia upekuzi mwili wa marehemu na kukuta pia karatasi kwenye mfuko wa suruali yake, ambayo Mwakajila aliandika Januari 2, mwaka huu, akimtuhumu mpenzi wake huyo kuwa amekuwa malaya na mlevi
 
Kamanda Malimi alisema polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajiki ya taratibu za mazishi.
CHANZO: NIPASHE

ELIMU BURE BADO KIZUNGUMKUTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Rais Dk. John Magufuli.
Wakati utekelezaji wa mpango wa elimu bure ya Rais Dk. John Magufuli, ukianza jana, baadhi ya wazazi wamekumbwa na sintofahamu baada ya wanafunzi kurudishwa nyumbani wakidaiwa michango na maeneo mengine utitiri wa wanafunzi ukiwa kikwazo, huku kwingine mwamko wa uandikishaji ukiwa chini.
Mwishoni mwa mwaka jana, serikali ilitoa mwongozi wa elimu ya msingi (shule ya msingi mpaka kidato cha nne) kuwa wazazi watatakiwa kununua sare za shule na michezo, madaftari, kalamu, chakula kwa wanafunzi wa kutwa na kugharamia matibabu ya watoto wao.
Ilisema, watatakiwa pia kulipia nauli ya kwenda shule na kurudi kwa wanafunzi wa kutwa na wa bweni wakati wa likizo, kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wanaosoma shule za bweni na wanaoishi katika hosteli zinazotumiwa na serikali.
Hali shuleni, ruvuma
Mkoani Ruvuma, baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Kutwa ya Nandembo iliyopo wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma, walifukuzwa kwa madai ya kushindwa kuwasilisha michango.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi hao wanaoishi hosteli iliyojengwa eneo la shuleni hapo kutokana na kuishi mbali na shule, walisema walifukuzwa kutokana na wazazi wao kushindwa kuchangia michango ya chakula, kusagia nafaka na michango ya kulipa mpishi.
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, kila mtoto ambaye amechaguliwa kusoma katika shule hiyo akiwa anatokea vijiji jirani, anatakiwa kuchangia debe nne za mahindi, moja la mpunga, kilo 30 za maharage, kilo mbili za chumvi, lita mbili za mafuta, Sh.10,000 kwa ajili ya kusagia mahindi na Sh. 5,000 za kumlipa mpishi wa shule hiyo.
Wanafunzi Waziri Seifu, Kadiri Ally na Fadhili Rajabu kutoka katika Kijiji cha Muhuwesi wanaosoma kidato cha pili katika shule hiyo walisema kuwa wanarudi nyumbani wakiwa hawana matumaini ya kurejea tena shuleni kuendelea na masomo yao kwa kuwa wazazi wao hawatawapatia michango hiyo hasa kwa kipindi hiki ambacho makwao wanakabiliwa na upungufu wa chakula.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa shule hiyo, Mary Ndunguru, alikiri kuwarudisha baadhi ya wanafunzi hao ili wakachukue chakula majumbani kwao kwa madai kuwa hali hiyo imetokana na shule yake kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto hao kwa kuwapatia chakula siku za masomo yao.
Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilayani Tunduru, Ally Mtamila, alisema ofisi yake kwa kushirikiana na ya mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya hiyo, walikwishapeleka taarifa za maelekezo kwa madiwani, waratibu elimu kata, yaliyowataka kufanya mikutano ya kufafanua maelekezo ya serikali juu ya utoaji wa elimu bure.
Mtamila aliendelea kufafanua kuwa kwa mujibu wa maelekezo hayo kutoka Tamisemi, fedha walizopokea kwa ajili ya utekelezaji wa elimu bure,  katika maelekezo ya fedha hizo za Rais Magufuli, hakuna maelekezo yanayowataka kuwahudumia wanafunzi wa kutwa chakula.
322 MBOZI WAKOSA MADARASA
Jumla ya wanafunzi 322 wa shule nne za sekondari waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, hawataanza masomo na wenzao kufuatia shule zao kukosa vyumba vya madarasa.
Ofisa Elimu Sekondari Wilaya yai Mbozi, Honsana Nshullo, alisema majina ya wanafunzi hao yamefichwa, mpaka pale wananchi watakapomaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa ndipo yatakapotolewa, ili waanze masomo na kuwataka madiwani katika maeneo husika kuharakisha ukamilishaji wa vyumba hivyo mapema ili wanafunzi hao waanze masomo haraka baada ya kufanya usaili wa pili.
Alizitaja shule hizo na idadi ya wanafunzi kuwa ni pamoja na Kilimampimbi wanafunzi 40 (chumba kimoja cha darasa kinahitajika), Nalyelye wanafunzi 88 (vyumba viwili vya madarasa), Mlowo wanafunzi 64 (vyumba viwili vya madarasa) na Insani wanafunzi 88 (vyumba viwili) na kwamba katika shule hii hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyechukuliwa.
Aidha, Nshullo alisema pamoja na kwamba serikali imefuta ada na michango mingine kwa wanafunzi lakini wazazi watakuwa na wajibu wa kuhakikisha watoto wanapata chakula cha mchana na mahitaji mengine kama vile sare, daftari na kalamu.
Manispaa ya Dodoma
Uongozi wa Shule ya Sekondari Mbabala iliyopo Manispaa ya Dodoma, umedaiwa kutoza Sh. 500,000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi anayelala shuleni (boarding).
Akizungumza na Nipashe, Mkuu wa shule hiyo, Gaitan Mwatenga, alikiri shule kutoza fedha hizo na kudai shule hiyo si ya bweni bali ina hosteli kwa wazazi wanaotaka watoto wakae shuleni hulipa fedha hizo.
Alisema kiasi cha Sh. 250,000 hutozwa kwa kila mwanafunzi anayekaa hosteli kwa muhula na kwa mwaka mzazi anatakiwa kulipa Sh. 500,000.
“Mimi sina bweni hapa, nina hosteli na shule zenye hosteli kwa hapa Manispaa ya Dodoma ni Mbabala, Mpunguzi na Hombolo yaani huwa kuna nafasi kidogo za hosteli kwa yule anayetaka kuja kukaa anakuja lakini anatakiwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya gharama ya chakula, wapishi, matroni, kuni na vitu vingine,”alisema mkuu huyo na kufafanua kuwa bodi ya shule ndiyo iliyopanga kiwango hicho ambacho ni sawa na mwanafunzi kutumia Sh.1,500 kwa siku.
Akifafanua suala hilo, Afisa Elimu mkoani hapa, Juma Kaponda, alikiri shule hiyo kutoza fedha hizo na kudai kuwa ni kwa ajili ya hosteli sio bweni.
Alisema kinachozungumzwa kwenye elimu bure ni kwa maana ya gharama za  uendeshaji na si bure kwa maana ya gharama za mtoto.
Mwamko hafifu simiyu
Katika Shule ya Sekondari Simiyu, iliyoko Kata ya Malambo, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, hadi juzi hakukuwapo mwanafunzi yeyote ambaye alifika kwa ajili ya kujiandikisha kuanza kidato cha kwanza.
Mmmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa shule, alisema hakukuwa na mwanafunzi yeyote ambaye amerejesha fomu zilizochukuliwa kwa ajili ya kujiunga na masomo shuleni hapo.
“Shule hii inatakiwa kupokea wanafunzi 220 na ambao wamechukua fomu mpaka sasa ni zaidi ya 100,  lakini hadi leo (juzi) hakuna hata mmoja ambaye amerejesha fomu kwani mimi ndiye napokea fomu hizo,” alisema.
Pia katika Shule ya Sekondari Kidinda, kata ya Bariadi, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Shija Mayunga, alisema wamepokea wanafunzi watatu tu ambao alisema walifika na fomu pamoja na mahitaji muhimu kwa ajili ya kuanza masomo.
“Mwitikio bado mdogo sana mpaka sasa tumepokea wanafunzi watatu tu na hapa hatuoni dalili za kupokea wanafunzi wengine lakini tuna matumaini hadi kufika mwishoni mwa wiki hii wanafunzi wanaweza kuongezeka,” alisema.
Mayunga alisema shule hiyo inatakiwa kupokea wanafunzi 253 na kuonyesha kushangazwa na wazazi kushindwa kuwapeleka wanafunzi shule wakati serikali imetangaza elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne.
Katika Shule ya Sekondari Biashara, kata ya Sima, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mathias Joseph, alisema hadi juzi saa 6:40 mchana walikuwa wamepokea wanafunzi 29 kati ya 337 wanaotakiwa kuripoti shuleni hapo kuanza kidato cha kwanza.
Alisema mwitikio wa wazazi kupeleka wanafunzi shule ni mdogo ikilinganishwa na matarajio yao baada ya serikali kuondoa michango ikiwamo ada.
Mwongozo wa elimu Bure
Mwongozo wa elimu bure uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, elimu msingi bila malipo, serikali ilikuwa igharamikie utayarishaji na uendeshaji wa mitihani ya kitaifa, uthibiti ubora wa shule, ruzuku ya uendeshaji wa shule ikiwamo ulinzi, umeme, maji na ununuzi wa chaki na karatasi pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.
Serikali pia itagharamikia kununua vitabu, kemikali na vifaa vya maabara, samani yakiwamo madawati, vifaa vya michezo, matengenezo ya mashine na mitambo pamoja na kujenga na kukarabati miundombinu ya shule.
Majukumu ya wazazi 
Kwa mujibu wa mwongozo huo, wazazi wanatakiwa  kununua sare za shule na michezo, vifaa vya kujifunzia vikiwamo madaftari na kalamu, chakula kwa wanafunzi wa kutwa na kugharamia matibabu kwa watoto wao.
Imeandaliwa na Anceth Nyahore, Simiyu, Bosco Nyambege, Mbozi, Stevie Chindiye, Tunduru na Augusta Njoji, Dodoma
CHANZO: NIPASHE

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao


Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya,  kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi




Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji

Waziri Ummy Mwalimu atembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

images 
Na Mwandishi Maalum
 WAZIRI WA AFYA Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili  

kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mifuko ya afya Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na Halmashauri na wananchi, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.

Ziara ya Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa NHC Ruvuma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Nyumba za gharama nafuu NHC Mkuzo Songea zinavyoonekana kwa sasa.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akimwelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Ruvuma, Saidi Bungara akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Pius Tibazarwa alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkuzo, Songea.

MAJALIWA: NAFARIJIKA KUONA WAZEE WANAPATA MATIBABU BURE TENA BILA USUMBUFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa amefarijika kuona wazee wanapata huduma za matibabu bure na kwa utaratibu mzuri katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza na madaktari, wauguzi na watumishi wengine wa hospitali hiyo wiki hii, alivyokuwa kwenye ziara mkoani humo, Waziri Mkuu  Majaliwa amesema  utaratibu wa kutenga chumba maalum chenye madaktari wawili  mahsusi kwa ajili ya kuwahudumia wazee  unaotekelezwa hospitalini hapo  umeondoa  adha kubwa  kwa wazee kusubiri matibabu kwa muda mrefu  jambo  ambalo ni kero kwao.

Amesema  kuwa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  imethibitisha kwamba    agizo la Serikali la kutaka  hospitali zote za Serikali  nchini ziwe na dirisha maalum kwa ajili ya wazee na  watibiwe bure linatekelezeka na kuzitaka hospitali zote nchini kuiga mfano huo.

 “Hospitali zote nchini  ziige  mfano wa hospitali ya  Mkoa wa Ruvuma kwa  kuwaheshimu wazee wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hizo kwa kuanzisha dirisha maalum kwa ajili yao kama agizo la serikali linavyosema na wasitozwe malipo ya aina yoyote” alisema Waziri Mkuu.

 Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa hata wanapokwenda kuchukuwa dawa uwekwe utaratibu wa kuwapa kipaumbele kwa kuwahudumia kwanza ili wasisubiri kwa muda mrefu. Na kusisitiza kuwa kibali maalum kinachowapa fursa wazee kutibiwa bure hospitalini hapo kindelee kutolewa na kiheshimiwe.

Awali, alitembelea chumba maalum cha wazee  ambapo Waziri Mkuu alipata fursa ya kuzungumza na Bibi Antonia Moyo  ambaye alisema hajawahi kutozwa fedha wala kukaripiwa  wakati wote alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu kupitia dirisha la wazee.

Waziri Mkuu Majaliwa, pia ametembelea wodi mbalimbali, chumba cha upasuaji pamoja na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma za Bima ya Afya.


WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA TUMBAKU MKOANI RUVUMA NA KUWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA SONAMCU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.



Akizungumza jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.
Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.
Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji. 
Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.


“Serikali imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.
Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.
Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo. 
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es Salaam. 
(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.

WAZIRI MKUU,KASSIM MAJLIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika kuwahudumia wagonjwa wao waliolazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti  Mwambungu.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo  Waziri Mkuu aliitembelea na  kuzungumza na watumishi  akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John  ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.
 Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU AKAGUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wialaya ya Songea lilipo katika kijiji cha Lundusi, Wilaya ya Peramiho mkoani Ruvuma. 

Alipowasili jana katika eneo hilo alikutana na viongozi wa jadi ambapo Mzee Daniel Gama alimkabidhi ngao na silaha ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kijijini hapo, pia alipata fursa ya kutazama ngoma ya mila ya kabila la Wangoni.

Mara baada ya kukagua jengo hilo la ghorofa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lundusi Bwana Rajabu Mtiula amesema jengo hilo lenye ofisi 50, vyoo 4, ukumbi mkubwa 1 na kumbi ndogo 2, ambapo mradi huo umetekelezwa kwa fedha za mfuko wa Mradi wa Maendeleo na Serikali. 
Hadi sasa Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 200 na utekelezaji wake umekamika kwa 85%, hivyo wanatarajia kuanza kutumia jengo hilo mwezi Februari, 2016.

Akizungumza jana (Jumatatu, Januari 4, 2016) na wananchi wa kijiji cha Lundusi, Waziri Mkuu, amewapongeza wananchi wa Lundusi kwa hatua hiyo ya maendeleo na kusema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Mkuu Majaliwa, ametaka kuwepo na mikakati ya uboreshaji wa eneo hilo kwa kusogeza huduma karibu ili kuvutia watu zaidi katika eneo hilo.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ametoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na Waziri Mkuu kwa kuchaguliwa na kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano.

Pia, ameishukuru Serikali kwa kusaidia kujenga jengo hilo, na pia ameeleza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo ikiwemo wakulima kutofaidika kwa bei ya soko ya kuuza mahindi, kutokuwepo na umeme na maji.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Waziri Jenista kufuatilia kero hizo kwa Wizara husika na baadae kuleta mrejesho kwa wananchi.

Waziri Mkuu Majaliwa anaendelea na ziara mkoani Ruvuma, leo siku ya jumanne (Januari 5, 2016) atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kuongea na Watumishi wa hospitali hiyo na baadae ataongea na Watumishi wa Umma.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, JANUARI 5, 2016.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA NFRA NA UJENZI WA OFISI YA MKURUGEZI PERAMIHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Maposele wilayani  Peramiho baada ya kukagua ujenzi wa  jingo la Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma  Januari 4, 2016. (PIcha na Ofisi a Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungungua tawi la Benki ya Posta la Songea akiwa katika ziara ya mkoa wa  Ruvuma Januari 4, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama .
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kadi ya akaunti yake ya Benki ya Posta Tanzania aliyokabidhiwa  baada ya kuifungua alipokuwa akifungua tawi la Benki hiyo la Songea Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassi Majaliwa akiagana na watuMishi wa Benki ya Posta, Tawi la Songea baada ya kufungua tawi lao Januari 4, 2016. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akivalishwa vazi la jadi la  Wangoni baada ya kuwasili kwenye   kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa  ngao silaha  na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa silaha za jadi na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya mila ya kabila la Wangoni wakati alipowasili    kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa