Mbunge wa Nkasi kaskazini Ally
Keissy amewataka wabunge waungane kukataa matumizi ya serikali kuwaleta
wakurugenzi,wakuu wa mikoa pamoja madereva kwenda Dodoma kushiriki
vikao vya Bunge kwani fedha nyingi hupotea bila mafanikio kuonekana.
Kessy ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11.
''Huu utaratibu wa kuwaleta
madereva, na wakurugenzi pamoja na wakuu wa mikoa ni lazima wabunge
tuungane kupinga matumizi yasiyo ya lazima,hapa na tuanze na hawa maana
kuwasafirisha wakuu wote hawa nchi nzima kuja Dodoma hizo fedha
zingeelekezwa katika sehemu nyingine kusaidia miradi ya
wananchi''Amesisitiza Kessy.
Aidha Kessy ameiomba serikali
kumuunga mkono jimboni kwake katika kwenda kuhakiki fedha zilizotumwa
kwa ajili ya miradi ya maji na mbolea kwa wakulima kwani fedha nyingi
zimeliwa.
0 comments:
Post a Comment