Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.
Akizungumza
na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni
(Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea,
Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna upatikanaji wa
masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa
wananchi.
Pia,
ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na
kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu
mmoja mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa
aliyopata.
“Nawapongeza
sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi
654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4
tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema
Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amesisitiza kilimo cha umwagiliaji katika maeneo
yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana
kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na
kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema zaidi ya asilimia 90
ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula
na biashara yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru
na Songea vijijini, korosho ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru,
Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijinina tumbaku maeneo
ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.
Alisema,
Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada
kwa kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa
nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 - 2016. Mahitaji yakiwa ni tani
469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za
ongezeko hilo la tani ni pamoja na matumizi ya dhana bora za kilimo,
matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo,
aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Waziri
Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya
kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho siku ya jumatatu atakuwa na
shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea,
kukagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda
ya Songea na kukagua Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kupitia
ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa
shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na
kuweka msisitizo katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta
ya Afya.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, JANUARI 4, 2016.
0 comments:
Post a Comment