Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha
mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha
Ushirika cha SONAMCU.
Akizungumza
jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa
Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku
wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa
Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru
Kaskazini.
Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha
kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni
katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua
viwanda nchini.
Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na
kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda
hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za
kuendelea na uzalishaji.
Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi.
Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda
hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote
wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na
kutaka wafikishwe Mahakamani.
“Serikali
imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki
vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu
huku akishangiliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima
wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya Ushirika
na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao hadi
kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.
Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi
ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao
wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800
kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na
uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit
Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.
Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa
linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa
na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na kuviendesha
Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya
ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na
kurejea jijini Dar es Salaam.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.
0 comments:
Post a Comment