Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANAWAKE wilayani Songea, Ruvuma wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko
ya kiuchumi hapa nchini kwa kuwa mfano bora katika kufanya kazi za
kujiletea maendeleo.
Wameelezwa wakifanya hivyo, itawawezesha kubadili mawazo na mtazamo
kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu anayehitaji kusaidiwa kwa kila kitu
katika maisha yake.
Mbali na hayo, wameaswa kutumia uwezo wao kuibadili jamii ya
kitanzania kitabia na kifikra dhidi ya mtazamo kwamba mtoto wa kike
ndiye anayeongoza katika suala zima la mmomonyoko wa maadili,
unaosababishwa na kuingia kwa utandawazi.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na diwani wa Ndilimalitembo katika
Manispaa ya Songea, Cresensia Kapinga, wakati akizungumza na wanawake
wajasiriamali wa kata hiyo wanaojishughulisha na biashara ndogo ikiwemo
matunda na mboga.
Alisema hivi sasa kuna vitendo vya mmomonyoko mkubwa wa maadili hapa
nchini ambapo vijana wanaiga mienendo ya kigeni na wakati na kuacha mila
na desturi ya Mtanzania, jambo ambalo ni hatari.
Kwa mujibu wa Kapinga ni kwamba vitendo hivyo vinahitaji nguvu ya
pamoja kwa wazazi na walezi na hata kwa jamii husika kwa sababu tayari
imeonekana katika baadhi ya familia mzazi anashindwa kukemea tabia hizo
na kusababisha vijana wengi kuangamia.
Alisema asilimia kubwa ya watoto wa kike wanaambukizwa virusi vya
Ukimwi na vijana wa kiume wanaingia katika matumizi zaidi ya dawa za
kulevya.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment