Mwandishi wetu, Songea
Hospitali ya Songea ambayo nitegemeo kwa wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma inakabiliwa na Changamoto ya Kukosa mashine ya kupiga picha x-ray kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa.
Hayo yamebainika baada ya watu 17 kupata ajali na kushindwa kupata huduma ya upimaji katika hospitali ya hiyo kutokana na mashine ya x-ray kuwa mbovu na kusababisha majeruhi kupelekwa hospitali ya Peramiho songea vijijini kilometa 24 kutoka songea mjini ili kwenda kupata huduma hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Songea Mathew Chanangula amesema katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mlima Mkwaya songea vijijini kati ya watu 17 walio pata ajali hiyo mtoto mwenye umri wa miaka 2 Daima Rashidi alifariki dunia baada ya kupoteza damu nyingi
Chanangula alisema wagonjwa waliokimbizwa katika Hospitali ya Peramiho na sabababu zilizomfanya kuidhinisha kwenda kutibiwa huko kuwa ni kutokana wengi kuvunjika mikono miguu na Majeraha makubwa ambayo yalihitaji vipimo vya x-ray ambavyo havipatikani hospitalini hapo.
Majeruhi hao ni wale walionusurika katika ajali iliyotokea barabara ya Mkenda-Songea Maeneo ya Mlima Mkwaya iliyosababishwa na mwendo wa Kasi na Gari aina ya Center iliyopinduka baada ya kukatika breki na kugonga Land Rover iliyo kuwa mbele yake.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment