Home » » CHADEMA NEWALA YAZOA 276 CCM

CHADEMA NEWALA YAZOA 276 CCM

na Andrew Chale
VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limeendelea kukichanganya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Newala, na kufanikiwa kuzoa wanachama 276.
Katibu wa CHADEMA, Wilaya ya Newala, Mhunzi Rashid, katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, alisema kuwa wananchi mbalimbali wengi wao wakitokea CCM, walifanikiwa kujiunga na chama hicho baada ya kufanya mikutano ya ukombozi kwenye kata tano na vijiji vyake vipatavyo 32.
“Tumetumia uwezo na elimu bora tuliyoipata kutoka kwa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA waliopata kutembelea mikoa ya kusini na pia walipofanya mikutano yao hapa imetutia ujasiri mkubwa, nasi kufanikiwa kupata wanachama hawa,” alisema Mhunzi.
Katika mikutano hiyo, Kata ya Kitangari waliweka kambi kwa siku saba na kufanya mikutano ya hadhara na kuvunja ngome ya CCM.
Mhunzi alitaja kata nyingine walizotembea katika jimbo hilo la Newala lenye kata 28 kuwa ni Mtopwa, Maputi, Nandwahi na Chiwonga.
Aliwataja baadhi ya vigogo ndani ya vijiji waliojivua gamba kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Azimio, na Mwenyekiti wa Kijiji cha Samora, aliyefahamika kwa jina la Mzee Mpotto.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa