Home » » NAMTUMBO WAMPATA MAKAMU MWENYEKITI

NAMTUMBO WAMPATA MAKAMU MWENYEKITI

na Stephano Mango, Songea
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wamemchagua Titus Ngoma kwa kura 24 kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo atakayeongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Steven Nana alisema madiwani katika halmashauri hiyo wapo 24 na wote kwa ujumla wao wamemchagua Diwani wa Kitanda kushika nafasi hiyo.
Nana alisema sheria na kanuni za mabaraza ya madiwani zinaeleza wazi kwamba Mwenyekiti wa Halmashauri akichaguliwa ataongoza kwa kipindi cha miaka mitano ila nafasi ya makamu mwenyekiti na kamati mbalimbali za madiwani zinachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.
Awali, nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Diwani wa Hanga, Kassim Ntala aliyeongoza kwa mwaka mmoja na kwamba awamu hii hakugombea nafasi hiyo.
Alifafanua kuwa, mchakato wa kumpata Ngoma ulianza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Namtumbo na kupelekwa mkoani kabla ya kurudishwa kwa ajili ya uchaguzi huo ambapo wagombea watatu walichuana.
Aliwataja waliokuwa wagombea kwenye kinyang’anyiro hicho na kura zao kwenye mabano kuwa ni Daniel Nyambo (4), Gidion Mpilime (6) na Titus Ngoma (14).
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa