Home » » VIWANJA 18,000 KUTOLEWA KWA WANANCHI

VIWANJA 18,000 KUTOLEWA KWA WANANCHI



na Julius Konala, Songea
KAMPUNI ya upimaji wa viwanja ya Ardhi Plan L.td inayofanya kazi zake katika Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inatarajia kugawa viwanja 18,000 kwa wananchi walioomba ili waweze kuviendeleza.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Gombo Samandito, alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa kata hiyo.
Alisema kuwa viwanja hivyo vitagawiwa kwa wananchi ambao waliomba kupimiwa kupitia kampuni hiyo kwa kuzingatia ramani inayostahili pamoja na kuwajali wale wenye makazi yao ya siku nyingi kubakia sehemu stahiki.
"Kampuni yangu imeweza kutatua kero iliyokuwa ikiwakumba wananchi tangu siku nyingi kufuatia suala la ardhi ambalo kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakilalamika kuishi katika makazi holela yasiyo rasmi kisheria,” alisema mkurugenzi huyo.
Alieleza kuwa kampuni yake imeisaidia serikali kukabiliana na kero zilizokuwa zikiwakabili wananchi na kubaki wakiilaumu serikali siku zote wakati uwezekano wa kulitekeleza upo.
Naye mkazi wa kata hiyo, Pumziko Mlelwa aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwaepushia migogoro iliyokuwa ikijitokeza katika ardhi na kueleza kuwa zoezi hilo litawasaidia kupunguza migogoro hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa