Mwandishi wetu, Songea.
Jumla ya Shilingi 1,500,000/= zilizotolewa na Mfuko wa Jimbo la Peramiho Songea Vijijini ili zisaidie vikundi vya Muungano na Kikundi cha Umoja katika Kijiji cha Mpandangindo Songea Vijijini hazijawafikia Walengwa.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Muungano Zeituni Msemwa na Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja Winifrida Mapunda, walisema kuwa wamepokea barua kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songeaya tarehe 28/06/2012 kumbukumbu namba DED/F,10/94/130 kufahamishwa kuwa Mfuko wa Jimbo umetoa Shilingi 1,500,000/= lakini walipouliza kwa Diwani Gotald Haule alikuwa hana majibu.
Mwenyekiti wa Muungano Zeituni Msemwa alipofanya uchunguzi amebaini kuwa fedha hizo zilizotolewa na Mfuko wa Jimbo la Peramiho zimechukuliwa na Diwani Gotald Haule akishirikiana na Mtendaji wa kijiji cha mpandangindo Songea vijijini kwa kughushi sahihi za wajumbe wa Muungano na Umoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Caseman Maswaga amesema uchukuaji wa fedha hizo umeshirikisha watu wawili wanaoaminiwa na Halmashauri ya wilaya ya songea , Mtendaji wa kijijij na Diwani wa kata ya mpndangindo hao ndio watu wa kwanza kuhojiwa kaimu mkurugenzi amesema tume ita tumwa ili kuwabaini wote walio husika ili sheria ichukue mkondo wake.
Afisa Mipango ambaye ni Katibu wa Uratibu wa Mfuko huo wa Jimbo la Peramiho Nema Hashimu amekiri kutoa fedha hizo kwa niaba ya Mkurugenzi bila kujua majina yaliyosndikwa ni ya wajumbe.
0 comments:
Post a Comment