Home » » WANAFUNZI SONGEA GIRLS WABAKWA KIMAZINGARA NA WANAUME

WANAFUNZI SONGEA GIRLS WABAKWA KIMAZINGARA NA WANAUME

Mwandishi wetu, Songea
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wameiomba Serikali kuwaongezea ulinzi kutokana na kufanyiwa vitendo vya kubakwa kimazingara nyakati za usiku.
Dada Mkuu wa Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Songea Janemary Mwinyikombo amesema tabia ya kuingiliwa kimwili mara mara na wanaume imeongeza hofu ya wanafunzi na kusababisha wanafunzi kushindwa kujisomea nyakati za usiku.
Janemary Mwinyikombo akiwa na Katibu wa wanafunzi Bernadetha Mathew Pamoja na Wanafunzi waliofanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kuchaniwa nguo kwa wembe na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Ankol ambaye mara kwa mara huingia kwa njia ya kimazingara wamesema hali hiyo inawakosesha raha shuleni hapo
Wamesema pamoja na wanafunzi kufunga milango na kupigilia misumari kwenye madirisha lakini cha kushangaza wanaume hao huingia na kuchana nguo za wasichana maeneo ya kifuani na sehemu za siri.
Rosemary amesema hali hiyo hutokea kuanzia saa saba usiku ambapo wanafunzi hao hukumbwa na hali ya kushindwa kusema pindi mwanaume huyo anapoingia bwenini.
Hata hivyo wameomba jamii na wazee wa mila kukaa na kuweza kulitatua tatizo hilo vinginevyo itasababisha wanafunzi kuathirika zaidi kisaikolojia jambo litakalo sababisha elimu kuporomoka shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Welinald Riki Liwiki amekiri kuwepo kwa Vitendo hivyo na amesema ameongeza ulinzi, yeye mwenyewe pia anashiriki ulinzi, ameomba Jamii kushirikiana na shule katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo kwa wanafunzi.
“Nimekuwa nikishiriki katika ulinzi wa usiku na nakumbuka siku moja nilinusurika kuuwawa na mlinzi wetu baada ya kudhani mimi ndiye mwanaume anaye waingilia wanafunzi kimazingara” amesema Liwiki
Shule ya Sekondari ya wasichana Songea kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na vitendo vya wanaume kuwaingilia wanafunzi kimazingara hali inayowafanya wanafunzi hao kuishi kwa wasiwasi na kukosa umakini wa kusoma shuleni hapo.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa