Home » » UFISADI MWINGINE: MIL. 70 ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI SONGEA ZAHUJUMIWA

UFISADI MWINGINE: MIL. 70 ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI SONGEA ZAHUJUMIWA

Adamu Nindi – Songea
 
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Mkoa wa Ruvuma TACIDS Emanueli Petro amesema atachukua hatua za kisheria kwa wale wote walio husika na ubadhilifu wa fedha zilizo tolewa na Water Read kwa ajili ya Kuwasaidia waathirika wa UKIMWI Mkoani humo.
 
Kauli ya Petro inakuja baada ya baada ya Uongozi uliokuwa ukiongozwa na Benardi Mapunda kubainika kufuja fedha zilizo letwa kupitia SHDEPH ambazo zilitolewa na wafadhili wa Water Read kutoka Mbeya kiasi cha shilingi 70milioni na ndoo 721 ambazo zilitolewa pia na PSI kupotea katika mazingira yasiyojulikana.

Petro alisema kutokana na kutojulikana kwa matumizi ya fedha hizo, ni dhahiri kuwa watuhumiwa hao walitumia pesa kinyume cha malengo tarajiwa na kwamba sheria ya UKIMWI ina ruhusu kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote ambaye ametumia fedha za mradi kinyume cha utaratibu.
 
Mkurugenzi wa SHDEPH + kutoka makao Makuu Da-es –salamu Joseph Katto alisema kumekuwa na tabia kwa watu wasio wanachama kujipachika kwenye SHDEPH + na kufuja fedha za waathirika na kwamba taratibu zinafanywa ili kuwabaini wanao husika na vitendo hivyo.
Maratibu wa SHDEPHA+ Mkoa wa Ruvuma Imedda Fussi na Makamu mwenyekiti wa SHDEPH+ Mkoa wa Ruvuma Philimini Chanaye wameiomba SerIkaLi kuwachukulia hatua watu ambao hawana huruma na roho za wenzao ambao wana ngoja faraja kutoka kwao lakini wao wanawahujumu
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa