na Stephano Mango, Songea
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, imewataka wananchi waliopimiwa ardhi yao katika Kata ya Mshangano kwa kutumia Kampuni ya Ardhi Plan, kulipia gharama za upimaji ili wengine waweze kuuziwa maeneo hayo na kuyaendeleza.
Wito huo ulitolewa jana na Diwani wa Kata ya Mshangano, Faustini Mhagama, wakati akiwahutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katani humo.
Mhagama alisema kuwa mradi ulioibuliwa na wananchi wa kata hiyo wa kurasimishiwa ardhi yao umekamilika kwa viwanja 18,000 kupimwa na hivyo wananchi wanapaswa kuvilipia haraka ili viweze kugawiwa Septemba 3, mwaka huu.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawapa fursa wananchi kuweza kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa, pia watatumia maeneo hayo kwa kupata mkopo na kuendesha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mshangano, alisema kuwa gharama za mradi huo zinatolewa na wananchi wenyewe kwa kutoa ardhi badala ya kusubiri.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment